Baada ya miaka miwili ya Mourinho Man United, huu ndio uamuzi mpya


Uongozi wa Club ya Manchester United leo January 25 2018 imetangaza maamuzi mapya juu ya kocha wao Jose Mourinho, ambaye ameifundisha club hiyo kwa takribani miaka miwili sasa.
Man United leo chini ya mtendaji mkuu wao Ed Woodwardwametangaza kumuongezea mkataba mpya Jose Mourinho, kocha huyo ambaye ana umri wa miaka 54 sasa ametangazwa kusaini mkataba mpya Man Unitedutakaomuweka Old Traford hadi 2020.

Jose Mourinho akisaini mkataba na Ed Woodward.
Jose Mourinho alijiunga na Man United mwaka 2016 miezi kadhaa baada ya kuondoka Chelsea na alisaini mkataba wa miaka mitatu amapo kabla ya kusaini mkataba mpya leo, mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwaka 2019.
Uamuzi wa Man United umekuja baada ya Mourinhokuiwezesha Man United kushinda EFL CupEuropa League, kuiwezesha timu hiyo kupata tiketi ya Champions League na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa EPL nyuma ya Man City.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post