Askofu amtaka Rais Magufuli atubu


BISHOP KAKOBE AMTAKA MAGUFULI KUTUBU.

Anaandika Anderson ndambo

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu""

Ameyasema hayo leo, katika ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge Da re salaam.

Akaendelea..."" leo ni siku ya watawala wa Tanzania, kutubu...leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa, amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu; tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja, na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizo jiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu, mara moja kupitia wabunge wenu wa ccm, si mko wengi"".

"""Sheria ni lazima zizingatiwe, na kwa hili nitapiga kelele mpaka mlima kilimanjaro"" huwezi kusema wewe huwezi kusemwa wewe ni nani?? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe??""

Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lkn anatukanwa na bado hatumii majeshi yake, hata wewe unaweza ukawa mvumilivu.

A. Ndambo

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post