Sammatha kuwa mchezaji bora Afrika

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta ametangazwa kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017.

Samatta ametajwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF leo kwenye orodha ya majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ambapo hii inakuwa ni mara ya pili kwa Samatta ambapo mwaka 2015 alitajwa kuwania tuzo hiyo kwa upande wa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.

CAF pia imetoa orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika ambapo mwaka 2015 tuzo hiyo aliitwaa Mbwana Ally Samatta baada ya kufanya vizuri akiwa na TP-Mazembe.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post