Robinho ahukumiwa kwenda Jela miaka 9


Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid, AC Milan, Man City na sasa anaichezea Atletico Mineiro ya kwao Brazil Robson De Souza maarufu kama Robinho, leo Alhamisi ya November 23 2017 amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela.

Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa kuwa miongoni mwa kundi la watu watano waliyohusika na kumdhalilisha msichana raia wa AlbaniaJanuary 22 2013 nchini Italia katika jiji la Milan, wakati huo Robinho na washikaji zake walikuwa Night Club.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post