UTAFITI: Umaarufu wa Rais Magufuli washuka kwa asimilimia 25%




Chanzo: #BBC Swahili
Rais John Pombe Magufuli
Umaarufu wa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli umeshuka kwa asilimia 25 kulingana na utafiti wa kura ya maoni iliofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa shirika la Twaweza lililofanya kura hiyo Watanzania 7 kati ya kumi wanaunga mkono utendakazi wa rais Magufuli ikiwa ni sawa na asilimia 71 ikilinganishwa na asilimia 96 mwaka 2016.
Hatahivyo ripoti hiyo ya Twaweza inaonyesha kuwa rais Magufuli bado ana umaarufu miongoni mwa watu wazima walio na umri wa miaka 52 kuendelea kwa asilimia 82 huku wale ambao hawana elimu ya kutosha wakimuunga mkono kwa asilimia 75 huku walio maskini wakimuunga kwa asilimia 75.
Miongoni mwa vijana walio chini ya umri wa miaka 30, ni asilimia 68 pekee waliomuunga mkono, asilimia 63 wakiwa wasomi na asilimi 66 wakiwa matajiri.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Twaweza Aidan Eyakuze, kushuka kwa umaarufu wa rais huyo kunaonyesha kupungua kwa uaminifu wa wapiga kura kuhusu wanasiasa wao.
''Kushuka kwa viwango hivyo pamoja na vile vya umaarufu katika kura ya maoni miongoni mwa wanaiasa kunatoa ujumbe kwamba raia wanaendelea kupoteza imani yao na viongozi wa kisiasa''.
Chama tawala cha CCM ambacho kimelitawala taifa hilo tangu 1962, kimesalia na umaarufu katika kipindi cha miaka mitano iliopita.
Baada ya umaarufu wake 2013 na 2014 kushuka kwa asilimia 54 kutoka asilimia 65 2012, chma hicho kinaendelea kuungwa mkono tangu uchaguzi ufanyike 2015 kwa asilimia 62 na asilimia 63 2017,kulingana na ripoti hiyo ya Twaweza iliotolewa siku ya Alhamisi.
Upinzani hatahivyo haujapata uungwaji mkono kama vile chama tawala.
Umaarufu wa Chama cha upinzani Chadema umeshuka kwa asilimia 17 katika kipindi kama hicho mwaka 2017 kutoka asilimia 32 2013.
Umaarufu wa CCM unatoka kwa wanawake, wakaazi wa mashambani ,watu wazima na masikini huku Chadema kikiungwa mkono na wanaume, vijana wasomi na wenye utajiri wa kadri.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post