Mshambualiaji ambaye ni mzaliwa wa Illiois James T Hodgkinson, mwenye umri wa miaka 66, aliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi na polisi.
Waliojeruhiwa ni pamoja na polisi wawili.
Hodgkinson alikuwa amemfanyia kampeni mgombea urais wa Democratic Bernie Sanders.
Bwana Sanders ambaye ni Seneta wa Vermont amesema amehusunishwa na kitendo hicho cha Hodgkinson.
Rais wa Marekani Donald Trump ametaja shambulia hilo kuwa la kinyama.
Hospitali ilisema kuwa Bwana Scalise alivunjika mifupa, na kupata majeraha ya viungo vya ndani na hivyo atahitaji upasuaji zaidi.
