Aibu! Siri nzito imevuja baada ya video chafu iliyomhusisha wakili
maarufu hapa nchini ambaye pia aliwahi kusimamia kesi ya Wema Sepetu,
Albert Msando na muuza sura katika video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift
Stanford ‘Gigy Money’.
Video hiyo inamuonyesha Msando akimshikashika sehemu nyeti msichana huyo
ambaye naye anajibu kwa kumkatikia mauno mwanasheria huyo msomi. Wakati
wadau mbalimbali wakimlaumu Msando kwa kile walichosema amejishushia
heshima, Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa ishu hiyo haikutokea kwa
bahati mbaya, bali ni kisasi kilichopangiliwa kwa ustadi.
MWANZO WA MCHEZO
Gigy Money alikuwa katika ziara ya kimuziki katika Wilaya ya Hai mkoani
Kilimanjaro akiwa na rafiki yake mmoja ambaye jina lake halikufahamika,
aliyekuwa akifanya mawasiliano na mwanasheria huyo maarufu nchini,
ambaye wakati huo alikuwa Arusha.
HUYU HAPA GIGY AKIMWAGA MBOGA…
Akizungumza baada ya video hiyo kuvuja, Gigy alisema wiki iliyopita
alikuwa na shoo maeneo ya Boma, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambako
akiwa huko alipata mwaliko kutoka kwa Msando wa kwenda kumtembelea
katika klabu yake iitwayo The Don, iliyopo Arusha.
“Kweli Msando nilikuwa sijawahi kuonana naye live, ila aliposikia nipo
Hai akanipa mwaliko, nikamwambia siwezi kwenda kwa kuwa nilikuwa bize na
shoo, pia sikuona umuhimu sana wa kumuona maana sicho kilichonipeleka.
“Baada ya kusema atanitumia usafiri, nikakubali, nilipomaliza kazi
alikuja na gari akiwa na watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili,
tulifika Arusha tukaenda club, nikalewa sana na baada ya hapo wakanipa
tena lifti kwenye gari yao kwenda hotelini.
“Tukiwa kwenye gari huku nimelewa, nilisikia Msando akimwambia mmoja wa
wale watu aturekodi nami sikuelewa ana maana gani, wakanishusha nikaenda
kulala peke yangu, sijalala na mtu yeyote, kesho yake nikaiona kwenye
mitandao, kiukweli kitendo hicho hakijanifurahisha hata kidogo,
kimeniudhi mno maana kimenidhalilisha,” alisema Gigy.
MSIKIE MSANDO SASA
Risasi Mchanganyiko lilijaribu mara kadhaa kumpigia simu yake ya mkononi
bila kupokelewa, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa simu,
likijitambulisha na kuomba kupata ufafanuzi kuhusu video iliyopo
mtandaoni, Msando alipiga simu na kuzungumza.
Risasi: Mambo vipi kaka!
Msando: Safi aisee.
Risasi: Pole kwa kilichotokea mzee.
Msando: Aaah ndiyo imeshatokea tena haina jinsi.
Risasi: Kwani ilikuwaje kaka?
Msando: Aaah, unajua kilichotokea ni kama huyu dada amenilipizia hivi!
Risasi: Kivipi? Msando: Si unajua huyu dada aliwahi kusema kuwa
hakumbuki ame-date na watu wangapi? Sasa mimi kuna siku nilipost
(kuandika katika mitandao ya kijamii) nikishangaa kama kwa miaka miwili
tu ameshawasahau, basi kuna tabu.
Sasa najua kuanzia pale akawa na hasira na mimi.
Risasi: Kwani mnafahamiana kabla ya leo?
Msando: Sijawahi kuwa na mawasiliano naye hata mara moja.
Risasi: Khaa, sasa kama hamjawahi kuwasiliana ilikuwaje ikawa kama vile ilivyokuwa?
Msando: Mimi nilikuwa nawasiliana na dada mmoja ambaye alikuwa anatumia
simu ya Gigy, aliniambia wanataka sana kuja kupaona klabu kwangu,
nikaona isiwe tabu, nikawakaribisha.
Risasi: Kwani wewe una klabu?
Msando: Ndiyo, inaitwa The Don, ipo Njiro.
Risasi: Aisee, safi kaka, uko vizuri. Enhee, ikawaje sasa?
Msando: Basi wakaja ile usiku sana, tukawa pamoja tunapata mambo, hadi kunakaribia kucha tukaondoka.
Risasi: Sasa ile video ilirekodiwa wapi?
Msando: Ndani ya gari wakati tunarudi, aliyekuwa anatupiga picha ni
rafiki yake. Risasi: Hukuelewa kama unarekodiwa au uliruhusu jambo hilo
lifanyike?
Msando: Aaah, si unajua tena mambo yale, sikufikiria chochote aisee.
Risasi: Lakini Gigy analaumu kuwa ni wewe ndiye uliyeingiza mtandaoni
ile video. Msando: No, ni namba ya Gigy ndiyo iliyoingiza mtandaoni.
Risasi: Kwa hiyo unafikiria kumchukulia hatua za kisheria Gigy? Msando:
Hapana, nina vitu vingi sana vikubwa vya kushughulika navyo kuliko
kushughulika na mtu kama Gigy, ninamuacha tu! Risasi: Dah, na vipi mke
wako ameshaiona?
Msando: Yes ameiona. Risasi: Vipi mapokeo yake?
Msando: Mke wangu ni sapota wangu namba moja, anajua baada ya pale
hakuna kilichoendelea, kwa hiyo iko vizuri. Mimi nina mke, watoto na
ndugu zangu na wa mke wangu pia, kwa hiyo hili jambo liko vizuri tu kwa
upande wangu.
Risasi: Sawa, lakini una wateja wako na watu wengine wanaokuheshimu, unawaambia nini kwa hili?
Msando: Nimeandika kwenye ukurasa wangu wa Instagram, unaweza kupitia.
Risasi: Asante, nitakutafuta kukiwa na ishu nyingine broo.
Msando: Asante karibu. Katika akaunti yake ya Instagram, Msando aliandika maneno haya kwa wateja wake, marafiki na watu wake
wa karibu. Nikikaa kimya nitakuwa mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea
hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao
nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is
we are all human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu.
Ni sawa, ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full
responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have
been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats
friendship. Kulikuwa na maneno katika baadhi ya mitandao, wakitaka Chama
Cha Wanasheria Tanzania (TLS) kumchukulia hatua Msando, kwani
amekidhalilisha. Lakini Risasi Mchanganyiko lilipofanya mawasiliano na
rais wa taasisi hiyo, Tundu Lisu alisema;
TUNDU LISU APIGILIA MSUMARI
“Msando ni mwanachama wetu, lakini sisi kama chama hatuwezi kumchukulia
hatua yoyote, angekuwa amefanya kosa hilo akiwa katika kazi zake za
kisheria, hapo sawa, lakini hili ni jambo binafsi. Wakili hazuiwi kunywa
pombe, hazuiwi kuchukua malaya, kwa sababu hayo ni mambo yake, ni juu
ya kanisa lake au mke wake kushughulika naye, siyo sisi.”
AJIUZULU
Wakati tukienda mitamboni, Wakili Msando alitoa taarifa ya kujiuzulu
nafasi yake kama Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, ambayo
aliielekeza kwa kiongozi wake mkuu, Mbunge wa
Kigoma Mjini, Zitto Kabwe. “Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha
uamuzi wangu wa kujiuzulu nafasi yangu kama Mshauri Mkuu wa Chama.
Uamuzi huu ni kutimiza hitaji langu la kuishi kama mfano kwa jamii
inayonizunguka. Kama kiongozi nastahili kuwajibika kutokana na video
clip iliyorekodiwa na kusambazwa. Ni wajibu wangu kwa chama changu na
nchi yangu kuwajibika kama kiongozi. “Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu
nikishirikiana nawe kujenga chama na kuhakikisha nchi yetu inaendelea
mbele.
Nakushukuru kwa kuniamini kwa kipindi chote tulichofanya kazi pamoja,”
alisema Msando katika taarifa yake. Zitto hakuchelewa kumjibu mshauri
huyo, akisema amepokea barua yake ya kuomba kujiuzulu nafasi yake na
yeye amekubali. “Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango
mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika.
Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kizalendo na mchango alioutoa. Ni
matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa
kadiri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama. “Nikiwa kiongozi
wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika
kujisahihisha kwake. Ndugu Msando Albert ameomba msamaha kwa jamii kwa
uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba,”
ilimalizia taarifa hiyo ya Zitto jana.