Njiwa ashikwa na mfuko uliojaa madawa ya Kulevya

Njiwa ashikwa na mfuko wa 'uliojaa madawa ya kulevya'

25 Mei 2017

Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya

Mshirikishe mwenzako

HakiAL-RAIImageMadawa hayo ya kulevya yalikuwa aina ya ketamine

Maafisa wa forodha nchini Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba madawa ya kulevya katika mkoba mdogo mgongoni, gazeti la Kuwait, la al-Rai limeripoti.

Jumla ya tembe 178 ziliipatikana katika mfukop huo uliokuwa umepachikwa mgongoni mwake, gazezi hilo lilisema.

Ndege huyo alinaswa karibu na jumba la forodha jijini Abdali, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq.

Njiwa akamatwa na polisi India

Mwanahabari wa Al-Rai alisema kuwa madawa hayo ya kulevya yalikuwa aina ya ketamine, nusukaputi ambayo pia hutumiwa kama dawa haramu katika sherehe.

Abdullah Fahmi aliiambia BBC kwamba maafisa wa forodha walijua mbeleni kuwa njiwa walitumiwa kusafirisha madawa ya kulevya, lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kunasa njiwa katika harakati hizo.

HakiAL-RAIImageMaafisa wa forodha wanaripotiwa kufuatilia njiwa huyo kabla ya kumshika

Maafisa wa utekelezaji wa sheria katika nchi nyingine, wamewahi kuripoti visa vya njiwa waliodaiwa kutumiwa kusafirisha madawa ya kulevya ya bei ghali japo kwa viwango vidogo.

Mwaka wa 2015, askari wa magereza jijini Costa Rica walimnasa njiwa aliyekuwa amebeba madawa ya kulevya aina ya kokeni na bangi kwa kipochi.

Unajua kwanini Flamingo husimama kwa guu moja?

Na mwaka wa 2011, polisi wa Colombia walimpata njiwa ambaye alishindwa kuburuka juu ya ukuta mrefu wa jela kwa sababu ya uzito wa mzigo wa madawa ya kulevya ya kokeni na bangi aliyopachikwa.

Njiwa wametumika kupeperusha ujumbe tangu enzi za Waroma, wakitumia uwezo wao wa kurudi nyumbani walikotoka.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post